Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Baada ya kuuawa kishahidi kwa Luteni Jenerali Amir Ali Hajizadeh katika shambulio la utawala wa Kizayuni, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amemteua Brigedia Jenerali Sayyid Majid Mousavi kuwa Kamanda mpya wa Kikosi cha Anga cha IRGC.
Katika amri rasmi ya uteuzi, Ayatullah Khamenei amesisitiza umuhimu wa: Kuimarisha uwezo wa makombora na ndege zisizo na rubani.
Kuendeleza teknolojia za anga za juu: Ili Kukuza maandalizi ya kiroho na uadilifu wa askari kulingana na roho ya Mapinduzi ya Kiislamu.
Aidha, Kiongozi Mkuu amemuelezea marehemu Jenerali Hajizadeh kwa heshima kubwa na kumuombea daraja ya juu peponi pamoja na mashahidi na Imam Ali (a.s), wakati wa salamu zake za Eid al-Ghadir.
Your Comment